Thursday, 31 July 2014

EID MUBARAQ TO YOU ALL


Nawatakia kila la kheri waislamu wote kwa kukamilisha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, na furaha tele na afya kwenu wote pamoja na familia zenu katika kushehrekea Eid .
EID MUBARAQ TO YOU AND YOUR FAMILY

Friday, 18 July 2014

PATA MUONEKANO WA HARUSI YAKO

pata muonekano wa harusi yako.










HATA SISI BONGO TUNAWAPAMBAJI WAZURI TUU AMBAO WANAUWEZO WA KUPENDEZESHA SIKU YAKO YA HARUSI. KWA KIDHUNGU WANAITWA WEDDING PLANNERS. 
MAMBO MAZURI YANAHITAJI MDA WAKO ,HIVYO TAFTA WAKO MAPEMA NA AKUPANGIE HARUSI YAKO .

Thursday, 17 July 2014

MISHONO YETU


Wasichana kwa wamama sasa tumekua tukipendelea zaidi kushona kushinda kununua nguo za dukani.ni vizuri zaidi kwani tumeweza kudumisha vya kwetu zaidi na kua kiafrika zaidi na kuacha umagharibi.
kwa msaada kuhusu mishono na ufundi wasiliana na mimi kwa no : 0716 666640 mda wowote napatikana.




kithuraah wa kaumo

UKOSEFU WA CHOO NA TIBA ZAKE

  • UKOSEFU wa choo ni tatizo sugu miongoni mwa watu wengi. Bila kujua kuwa ni tatizo ambalo linahitaji tiba ya haraka, watu wengi hupuuzia na kuona siyo tatizo kubwa na ni hali ya kawaida. Ukosefu wa choo wa muda mrefu, huwa ndiyo chanzo cha magonjwa mengine hatari
  • Mtu anapokosa choo kikubwa kwa siku kadhaa, uchafu hujikusanya tumboni na unapokosa sehemu ya kutokea hukimbilia kwenye damu na kuingia kwenye mfumo mzima wa damu. Uchafu huo unapoingia kwenye mfumo wa damu huwa sumu na chanzo cha maradhi mengine ambayo hujitokeza baadae na kuanza kumuathiri mtu, bila kujua chanzo chake.

  • Kwa kawaida mtu unapaswa kupata choo cha uhakika japo mara moja kwa siku, kutegemeana na mlo wake wa kila siku, unapokosa choo kwa siku nzima ili hali una kula milo yote kwa siku, elewa una tatizo katika mfumo wako wa kusaga chakula hivyo unapaswa kuchukua hatua haraka.

    MTU MWENYE TATIZO HILI ANA DALILI GANI?
    Mtu mwenye tatizo la ukosefu wa choo huwa na dalili kadhaa, ikiwemo kutumia nguvu na muda mwingi wakati wa kujisadia haja kubwa. Pili ulimi wake huwa na utandu mweupe na hutoa harufu mbaya mdomoni. Mtu huyu pia hukosa hamu ya chakula na wakati wote tumbo huwa limejaa.

    NINI HUSABABISHA TATIZO?

    Tatizo la ukosefu wa choo husababishwa zaidi na ulaji mbaya wa vyakula, kuacha kula matunda na mboga na staili mbaya ya maisha ikiwa ni pamoja na kutokunywa maji ya kutosha kwa siku.

    NINI KIFANYIKE?
    Ili kuondoa tatizo kabla halijawa sugu, fanya moja miongoni mwa haya yafuatayo: Kunywa maji ya uvuguvugu asubuhi mapema, kisha tembea tembea, baada ya muda utasikia haja ya kwenda chooni. Ili usifanye haraka na upate muda wa kutosha kujiandaa kwenda kazini, amka mapema zaidi. Kula kiasi cha kutosha cha salad ya mboga mboga na juisi ya matunda halisi asubuhi kabla ya kula chochote.

    Kila siku kabla ya kwenda kulala, kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na kijiko kimoja cha asali. Kunywa maji ya uvugu

    yaliyochanganywa na limau asubuhi na mapema kabla hujala kitu chochote. Kunywa ‘castor Oil’ muda mfupi kabla ya kwenda kulala. Ili

    kujiepusha kabisa na tatizo la ukosefu wa choo, jenga mazoea ya kunywa maji mengi, kula mboga na matunda kwa wingi kila siku na

    kuacha kabisa ulaji wa vyakula vilivyoondolewa virutubisho kama vile mikate myeupe, ugali wa unga mweupe, keki vyakula vyenye sukari nyingi na vyakula vingine vitamu.

     

    HIVI NDO VYAKULA VINAVYOHITAJI KULA ILI KUEPUKA NA KUONDOA TATIZO LA KUKOSA CHOO

Wednesday, 9 July 2014

10.07 KUMBUKUMBU YA MIAKA 12 YA BABA YANGU AMIRI HUSSEIN KAUMO



siku kama ya leo 10.07.2002, ni siku ya majonzi sana kwangu kwani ndio siku baba yangu kipenzi Mr. AMIRI HUSSEIN KAUMO alifariki ,ni miaka 12 sasa tangu tupatwe na msiba huu , naimani huko uliko uko pahala pema.ulikua Baba mzuri, rafiki mzuri sana kwangu ukiniongoza vyema ktk kipindi chote cha uhai wako,ukinifunza mengi mengi na kusisistiza zaidi kwenye elimu. kwa hilo nasema Ahsante sana.

nnamengi ya kusema lkn naomba niseseme mengi zaidi, nakupenda baba yangu na utaendelea kuwepo katika mawazo,akili na moyo wangu kila siku za maisha yangu. nakuombea salama huko uliko, Mmungu akupe kauli njema huko uliko, akupunguzie adhabu , akuweke mahala pazuri kwani hata mimi nakuombea salama huko uliko Baba yangu .

nakukumbuka sana, natamani ungekua nami hadi leo hii ukaona jitihada zangu katika kutafuta na imani hata huko uliko unaona na unajivunia kwa njia moja au nyingine ..
namshukuru Mmungu kwa kipindi chote hichi nimekua na afya njema na kila kitu kinaendelea sina budi kusema ""alhamdulillah""

MMUNGU AKULAZE MAHALA PEPA PEPONI BABA YANGU AMIRI HUSSEIN KAUMO


Monday, 7 July 2014

CHECK VIDEO MPYA ZA DIAMOND BUM BUM NA MDOGO MDOGO

BUM BUM VIDEO DIAMOND FEAT INYANYA
MDOGO MDOGO VIDEO
kama alivyoahidi ,Diamond Platinumz aachia video mbili kali ,waeza zicheki kupitia hapa .

DIAMOND AMSUPRIZE MAMA YAKE GARI YA MIL 38

katika hali ambayo hamna aliyewahi kufkiria mwanamuziki wa kimataifa wa Bongo Fleva Diamond Platinumz amshangaza mama yake katika siku yake ya kuzaliwa ambapo mama huyo ametimiza miaka 55 kwa kumzawadi gari aina ya Toyota Lexus new model yenye thamani ya Milion 38.1 za kitanzania.
mwanamziki huyo mbaye bado yupo nje ya nchi kikazi athibitisha kukabidhi zawadi hiyo kupitia meneja wake Babu Tale na kuikabidhi rasmi hiyo tar 07.07.2014.

MUONEKANO WA GARI KWA NYUMA

MUONEKANO WA GARI KWA MBELE
 
WEMA SEPETU AKIWA NA MKWEWE MAMA NASEEB ABDUL ''DIAMOND''

Wednesday, 2 July 2014

RAMADHAN WISHES 2014



MAY THIS RAMADHAN BE THE MONTH OF BLESSING, MONTH OF FORGIVENESS AND GUIDANCE FOR YOU AND YOUR FAMILY.