Monday 1 April 2013

ZAIDI YA WATU 20 WAFARIKI KWA KUFUNIKWA NA KIFUSI ARUSHA

WATU zaidi ya 20 wamefariki dunia kwa kufukiwa na kifusi wakati wakichimba mchanga aina ya Moramu katika machimbo yaliyopo Moshono nje kidogo ya jiji la Arusha.

Tukio hilo ambalo limegubikwa na simanzi na vilio kwa ndugu jamaa na wananchi,limetokea leo majira ya saa 5 asubuhi wakati marehemu hao wakichimba na kupakiaMoramu hiyo kwenye magari .

Pamoja na vifo hivyo magari mawili aina ya Fuso na Scania yameharibiwa vibaya baada ya kufukiwa na kifusi kilichoporomoka umbali unaofikia mita 50 kutoka usawa wa bahari.

Tayari kikosi cha uokoaji ambao ni Jeshi la Wananchi Kambi ya Tanganyika Parkers kimefanikiwa kuopoa miili ya marehemu 16

waliofukiwa.Baadhi ya miili ya marehemu imetambulika kwa majina kuwa ni Alex Maliaki, Gerald

Hamis, Sauli Rafael (Mbu), Barick Loselian,Kababuu Lowasale, Mwenda Kibobori, Japhet Mjivaine na Garald Masai.

Taarifa za mashuhuda zimebainisha kwamba chanzo cha kuporomoka kwa kufusi hicho ni mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Arusha zilizosababisha kukatika kwa Ngema baada ya kuzidiwa na maji ya mvua.



Chanzo cha habari Global Publishers

Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.

JUMLA YA MAITI 34 ZAPATIKA KATIKA AJALI YA KUANGUKA KWA JENGO

Kama tulivyopata habari mnamo tar 29/03/2013 jengo ambalo lilikua bado kwenye ujenzi kuanguka na kusababisha maafa ya watanzania wenzetu na wengine kujeruhiwa vibaya,uokoaji wa miili iliyobakia chini umemalizika leo na kutimia idadi ya watu 34 na vichwa viwili ambavyoo viwiliwili vyake havija patikana na kuleta jumla ya maiti 36.

Ni msiba mzito na tunawapa pole ndugu jaama na marafiki walofikwa na janga hili .

Pamoja na hilo leo mjini Arusha limetokea janga linalofanana na hilo katika machimbo ya kokoto baada ya kufukiwa na udongo wakati wakiwepo machimboni ,idadi kamili sijaijua tutapeana taarifa.

RIP wote walofikiwa na ajali hizi mungu ibariki Tanzania..



Kithuraah

Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.

Happy Easter

Nawatakia sikukuu njema ya pasaka..

Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.