Monday 17 November 2014

MATUMIZI YA MAFUTA YA NAZI NA UREMBO




Mafuta ya nazi ni mazuri kama yatatumika ipasavyo.yana uwezo wa kukufanya uonekane mrembo mwenye ngozi ya kuvutia.

MAKE UP REMOVAL/KUONDOA MAKE UP

mafuta ya nazi yanaweza pia kutumika kuondoa makeup usoni baada ya kutoka kwenye sherehe ukiwa na makeup unashauriwa kuitoa kabla ya kuingia kulala ili kuendelea na ngozi nzuri yenye afya.
mafuta ya nazi yanatumika hivi
chukua pamba safi chovya kwenye mafuta ya nazi.
kisha anza kufuta uso wako taratibu kwa kutumia pamba iliyo na mafuta ya nazi.
baada ya kufuta chukua cleanser uliyoandaa au nawa uso wako vizuri na sabuni.
ukifanya haya utasaidia kutunza uso wako na kuwa na afya nzuri.

KULAINISHA NGOZI

Mafuta ya nazi pia hutumika kama kilainishi kwa ngozi yako especially :
kuondoa magaga kwenye nyayo za miguu
kuzuia mipasuko ya nyayo za miguu
kukauka kwa ngozi ya mikononi
hivyo mafuta yanazi yanasaidia kwa kiasi kikubwa sana kulainisha ngozi na kuipa afya nzuri.

KUONDOA NGOZI ILIYOHARIBIKA/DEAD SKIN

Mafuta ya nazi husaidia kuondoa ngozi iliyoharibika katika mwili wako, ki hivii
chukua mafuta ya nazi, sukari na chumvi changanya upate mchanganyiko mmoja
kisha paka mwili mzima.
fanya massage kwa mchanganyiko huo kaa nayo kwa mda kisha kaoge vizuri na sabuni.
utaona tu mabadiliko katika ngozi yako baada ya zoezi hili.
fanya mara 3 kwa wiki au utakavyoamua wewe.

KUSAIDIA KATIKA KUNYOA/SHAVE OIL

Wengi wetu tumezoea kutumia Save cream wakati wa kunyoa nywele katika maeneo maeneo lakini mafuta ya nazi pia yanaweza tumika hapa balaya ya shave cream, yenyewe yanasaidia kutibu vipele vinavyojitokeza baada ya kunyoa.
haya mafuta wengi wanatumia katika kunyoa vinyweleo, inakuacha ukiwa soft na inasaidia kwa kiasi kikubwa kukufanya ngozi yako iwe salama tofauti na kutumia kiwembe au kitu kingine.

KUKUZA NYWELE

mafuta ya nazi, yanatumika katika kurutubisha nywele na kufanya ziwe na nuru na kujaza,
kupaka kwenye ngozi
kupaka sehemu ya nywele ambazo hafifu au zilizo katika.

Mafuta ya nazi yanapatikana kwa Kithuraah Collections
wasiliana nami kwa namba 0716 666640
kwa mahitaji ya mafuta ya nazi
na bidhaa nyingi za urembo






No comments:

Post a Comment