Monday 16 January 2012

JUA JINSI YA KUTENGENEZA JUICE YA UKWAJU NA FAIDA ZAKE KTK MWILI

Tulio wengi tunapenda kutumia ukwaju japo wachache sana hawapendelei wakidai kwamba unakwangua utumbo na kuweza kuababisha vidonda vya tumbo 
,lkn hapana ukwaju unafaida sana kwa afya zetu ,mimi binafsi na upenda sana japo nakumbuka kipindi cha miaka hiyo bado niko mdogo unapita kigengeni unanunua unaweka chumvi unakula co hivyo tuu ,bali unaweza kutengeneza juice ukanywa.

ukwaju(tamarind)
UANDAAJI WA JUICE YA UKWAJU
Juice ya Ukwaju

 Nunua ukwaju unapatikana sana sokoni
  • andaa maji kwenye dishi na uoshe kidogo tuu 
  • baada ya kuuosha chukua ukwaju wako weka kwenye sufuria yenye maji ya saizi na injika jikoni 
  • uache uchemke hasa ht kwa dakika 10/15 ili uuwe vijidudu 
  • ipua ukwaju wako jikoni na uache kwa muda upoe 
  • andaa maji yako masafi na chujio ili uweze kuchuja juice yako kwa uangalifu zaidi ili upate juice yenyewe
  • weka sukari kwa kiasi unachopendelea 
  • pia ili kupunguza ukali unaweza ukaweka hiliki au vanila ili kupata taste 
  • weka juice yako kwenye fridge ili ipoe tayari kwa kunywa 



Faida 10 za ukwaju:


  1. Chanzo kizuri cha viuasumu mwilini 'antioxidants' ambavyo huzuia Saratani (cancer)
  2. Chanzo cha Vitamini B na C vile vile "carotentes"
  3. Hushusha joto la mwili na kuondosha homa, hasa homa ya malaria na homa ya matumbo
  4. Huulinda mwili dhidi ya mafua na kero za mafua kooni
  5. Husaidia myeyusho na mmengenyo wa chakula na kuondosha kuvimbiwa
  6. Husaidia kutibu matatizo ya nyongo (bile disorders)
  7. Husaidia kurahisisha choo (laxative)
  8. Husaidia kupunguza wingi wa lehemu (cholesterol) na hivyo kuimarisha moyo
  9. Husaidia ngozi kuwa nyororo, vile vile husaidia ngozi inayopona baada ya kuungua au yenye vidonda
  10. Husaidia kuua minyoo tumboni (kwa watoto wadogo)

NB: Ikiwa ukwaju na asali havikudhuru, basi changanya hivyo viwili ili kupata faida maradufu!

13 comments:

  1. hapa nimejifunza kitu kikubwa sana,though kuhusu sukari haishauriwi sana better to use asali kwa afya zaid,thx

    ReplyDelete
  2. Asante sana kwa elimu hii adwim,mungu akujaalie.Nina matatizo kibao yanayotibiwa na ukwaju.Zamani niliona kama tunda pori tu.

    ReplyDelete
  3. Karibu dia ,na uendelee kujifunza mengi kupitia kithuraahtz blog.

    ReplyDelete
  4. Somo zuri lenye faida ndani yake

    ReplyDelete
  5. Thanks so much for your good information

    ReplyDelete
  6. God bless you kwa elimu nzuri kwa kweki

    ReplyDelete
  7. Barikiwa saaana kwa somo zuri

    ReplyDelete
  8. Asante sana ubarikiwe nimeelewa vzr juice ya ukwaju Na faida yake

    ReplyDelete
  9. Kuanzia leo naanza kutumia ukwaju

    ReplyDelete
  10. Mimi nikinywa ukwaju tumbo linauma

    ReplyDelete