Friday 16 January 2015

UTUNZAJI NA UREMBO WA MIDOMO/LIPS

Tukirudi kwenye safu yetu ya urembo, leo tujue jinsi gani ya kuremba mdomo yako na kuweza kuifanya yenye mvuto zaidi kwa wanaokutazama.

midomo ni sehemu muhimu sana katika kukamilisha unadhifu na muonekano mzuri
Ngozi ya midomo ni laini sana na inahitaji uangalizi katika kuitunza na kuifanya iwe mizuri zaidi.

utunzaji wake wala hauhitaji mambo mengi sana ni kidogo tuu.

Epuka kuacha midomo ikawa mikavu kwa mda mrefu kwani inasababisha kukatika na kuweka gamba gumu kwa juu.
hvyo jitahidi kutumia mafuta laini ya midomo/ vaselline / ama mafuta mengine mazuri ya mgando ambayo yanafaa kulainisha midomo yako.

vilainishi hivo nlivotaja hapo juu vitasaidia kulainisha midomo yako na kuifanya iwe na afya njema na sio yenye kukauka.

zoezi la upakaji wa vilainishi hvyo linashauriwa liwe , usiku wakati wa kulala paka mafuta yako mdomoni inasaidia kuamka ukiwa na lipsi laini na nzuri na pia akti wowote ambao utahisi lipsi zako zimekauka unatakiwa upake vilianishi hivi.

then ukipaka vilainishi ndio utaweza rembesha midomo yako kwa lipstick mbalimbali kutegemeana na skin tone yako au rangi ambayo umependezewa kuipaka siku hiyo.




JINSI YA KUPAKA LIPSTICK

  • Anza kwa kupaka kilainishi kabla ya kupaka lipstick yako. LipBalm
  • Paka Lip Liner ya colour ya lipstick ambayo unatarajia kupaka au kwa colour yeyote utakayopendezewa nayo.
  • Chukua lipstick yako pakaa ukianzia lips za chini ukifuatiwa na za juu na kuichanganya vizuri.
  • Kama unapendelea mg'ao zaidi unaweza kupaka lipshine kwa juu kung'arisha midomo yako.
  • Baada ya kufata steps hizo hapo, utakuwa umekamilisha upakaji mzuri wa Lipstick katika midomo yako na kuifanya ya kuvutia.

ZINGATIO

Angalia sana lipstick unayopaka na rangi ya ngozi yako. kwani kunalipstic nyingine zinachagua rangi ya ngozi.

Kwa mahitaji ya lipstick, lipliner, wanja , poda wasiliana nasi kupitia no 0716 666640. instagram @kithuraah.
karibuni wote.

No comments:

Post a Comment