Wednesday 7 January 2015

MISS BUMBUM 2012- BRAZIL AOZA MISULI KWA AJILI YA KUONGEZA MAKALIO


Miss Bum Bum 2012 huko nchini Brazil kwa jina la Andressa Urach amekumbwa na majanga ya kuoza misuli ya mapaja hii yote ni kwa sababu ya kuchoma sindano ya kuongeza makalio na mapaja yake kipindi cha miaka mi3 nyuma,


mrembo huyu mwenye umri wa miaka 27 alikua mwanariadha nchini humu na mwisho aliishia kwenye mashindano ya urembo.mrembo huyu alikaa wodini kwa mda wa mwezi mzima akihofia kupoteza mguu wake wa kushoto baada ya misuli kuoza na kumsababishia maumivu makali sana.
mrembo huyu aliziona picha zake zilizochukuliwa kipindi yuko mahututiambazo zilionyesha jinsi alivotobolewa tobolewa na kubandikwa plasta.

Miongoni mwa surgery ambazo amewahi fanya mrembo huy ni pamoja na , kuongeza matiti, kunyoosha pua, kupunguza mashavu ya shehemu za siri na nk.
Imethibitika kuwa Brazili ni moja ya nchii inayoongoza kwa watu wengi walio fanyiwa upasuaji wa mwili(Plastic Surgery).
mrembo huyu ameonesha kuwaogopesha wengi kutokana na madhara aliyoyapata kwa ajili ya upasuaji uliofanywa kwenye mwili wake.

Haya wale warembo wetu mnaopenda urembo kupitiliza kushinda jinsi alivokupanga MwenyeziMungu na kuongezea vya kuongeza haya ndio madhara yake sasa so just be natural jamani nini tena unaongeza ili iweje sasa kwa mfanoo.. na haya ndio matokeo yake sasa..

No comments:

Post a Comment