Thursday 5 February 2015

BOBBY KRISTINA MAHUTUTI KWA AJILI YA MADAWA YA KULEVYA

Ule usemi usemao maji hufuata mkondo unauhalisisa wake.
mtoto wa aliyekua Muimbaji Maarufu dunian Marehemu Whitney Houston naye aangukia katika janga la madawa ya kulevya na kusababisha hali yake kua mbaya baada ya kukutwa amezimia ndani ya Jacuz baada ya kulewa na madawa.

katika mazingira hayo alokutwa Bobbi Kristina akiwa amezimia ndani ya maji na kuwahishwa hospital kwa ajili ya uchunguzi na matibabu, ni sawa na mazingira ambayo alikutwa mama yake Whitney Houston akiwa tayari ameshafariki huku akiwa ameinamisha kichwa kwenye maji.

Kwa tukio la juzi, tovuti ya CNN iliarifu kuwa binti huyo wa mwanamuziki Bobby Brown alifikwa na hali hiyo mwishoni mwa wiki huku ndugu yake wa karibu akimweleza mwandishi wa tovuti hiyo, Sunny Hostin kwamba baada ya kugonga mlango mara kadhaa bila majibu, alipata shaka na kuingia ndani na kumkuta Bobby katika hali hiyo na kupiga simu polisi, ambao walifika na kumkuta akiwa na hali mbaya kisha kumpeleka katika Hospitali ya North Fulton.
Msemaji wa Polisi, Lisa Holland aliiambia tovuti hiyo kuwa walipofika walimkuta Bobby hapumui, lakini baada ya kufikishwa hospitali na kupatiwa huduma ya kwanza alianza kupumua, ingawa alikuwa hajitambui.
Tovuti ya TMZ imeripoti kuwa baada ya Polisi kufanya ukaguzi walikuta dawa za kulevya.
Kwa mujibu wa TMZ, siku moja kabla ya tukio Bobbi Kristina alikuwa na rafiki yake Maxwell Byron Lomas, ambaye mwezi mmoja uliopita alikamatwa kwa kusambaza dawa za kulevya na kuwekwa chini ya ulinzi na baadaye aliachiwa kwa dhamana.
Taarifa kutoka Polisi zinazoandikwa katika jarida la Fulton County Jail records zinasema Lomas amekuwa akihusishwa na kashfa ya dawa za kulevya kwa muda mrefu na siku moja kabla ya tukio hilo alikuwa na Kristina pamoja na mumewe Gordon.
Ilivyokuwa kifo cha Whitney
Whitney Huston alifariki dunia Februari 11, 2012 katika Hoteli ya Beverly Hilton jijini Los Angeles, saa chache kabla ya kufanya onyesho kwenye sherehe za maandalizi ya Tuzo za Grammy.
Mkuu wa Polisi wa Beverly Hills, Luteni Mark Rosen alithibitisha kukutwa kwa aina fulani ya vidonge vya kutuliza maumivu katika chumba alichofia mwanamuziki huyo, huku kukiwa na ushahidi kuwa alikuwa akitumia dawa za kulevya baada ya kushindwa kutumbuiza jukwaani mara kadhaa na kukaa kimya ‘akisikilizia’ kama wafanyavyo mateja.
Whitney ambaye alikuwa gumzo miaka ya 1980 na 1990 kutokana na sauti yake ya kumtoa nyoka pangoni na baadaye kwenye ushiriki wake katika filamu za ‘The Body Guard’ na ‘Waiting to Exhale’ aliwahi kukaririwa akisema baada ya kuanza kuyumba kwa afya yake: “Nina shetani mkubwa ananiandama, kama siyo marafiki zangu, basi ni maadui zangu au ni akili yangu inayonituma kufanya vitu ambavyo vitagharimu maisha yangu.”.



No comments:

Post a Comment