Tuesday 31 July 2012

MAPISHI YA VIBIBI


 MAHITAJI

1.Mchele Vikombe 2 
2. Tui la nazi  Kikombe 1 na nusu
3. Mafuta kijiko 1 cha chakula
4. Hamira Vijiko vya chai   2
5. Unga wa ngano kijiko 1 cha chakula
6. Hiliki  kiasi upendavyo
7. Sukari  Kikombe 1
JINSI YA KUANDAA 

1·  Osha na roweka mchele usiku mzima ndani ya maji baridi.
2·  Mimina vifaa vyote isipokuwa sukari , ndani ya mashine ya kusagia (blender) na usage mpaka mchele uwe laini.
3·  Mimina ndani ya bakuli na ufinike , kisha weka pahali penye joto ili mchanganyiko ufure.
4·  Ukishafura , mimina sukari na changanya vizuri ; ukiona mchanganyiko ni mzito sana, ongeza maziwa kidogo.
5·  Weka chuma kipate moto.
  Paka mafuta au samli kidogo kwenye chuma kisha mimina mchanganyiko kiasi kuunda duara na ufunike.
  Utazame ikishaiva upande mmoja , geuza upande wa pili mpaka iwe tayari.
  Endelea Mpaka umalize mchanganyiko wote,panga kwenye sahani na tayari kuliwa.
VIBIBI KATIKA PICHA.
 ENJOY YOUR MEAL

PISHI LA KATLES

MAHITAJI

1. Viazi Ulaya  Nusu Kilo
2. Kitunguu swaum Kikubwa 1
3. Myama ya kusaga Robo 
4.Limao
5.Vitunguu Maji Vikubwa 3
6. PiliPili Manga 
7. PiliPili mbuzi
8. Mayai 2
9. Mafuta kiasi
10. chumvi.
11.unga wa ngano kikombe 1

JINSI YA KUANDAA

menya viazi vyako na uvioshe vizuri kwa maji safi
weka kwenye sufuria na uweke chumvi kiasi 
weka jikoni vichemke hadi viwe laini .
wakati viazi viko jikoni andaa nyama yako ya kusaga 
weka chumvi,ndimu,swaum,tangawizi,na pilipili manga,na km utapenda kuweka pilipili mbuzi 
katiakatia vitunguu maji  na uweke jikoni nyama nayo iwive.
viazi vikiwa tayari mwaga maji na uhakikishe hamna maji na uanze kuviponda hadi madonge yaishe.
nyama ikiwa tayari epua na uweke pembeni ipoe.
weka ndimu ktk viazi vilivyopondwa pamoja na pilipili manga kiasi changanya kwa pamoja.
tengeneza shape ya duara ukiweka kishimo kati kwa ajili ya kuweka nyama ya kusaga.
tengeneza madonge yako huku ukiweka nyama kati na kufunga kwa kutumia viazi vilivyopondwa.
baada ya kumaliza madonge yote .
andaa mayai kwenye kibakuli na uyachanganye alafu weka chumvi.
weka mafuta jikoni yachemke
then chukua donge moja moja zamisha kwa unga wa ngano (husaidia kutokuvurugika) halafu dumbukiza kwa mchanganyiko wako wa mayai na uweke kwenye mafuta.
kaanga hadi vibadilike rangi ,
katlesi zako ziko tayari kwa kuliwa..
na katlesi zako zitakuwa hivi katika picha.


ENJOY YOUR MEAL.

JIFUNZE MAPISHI MBALI MBALI YA FTARI KUPITIA HUMU

Wadau kwa huu mwezi mtukufu wa ramadhani tujifunze mapishi mbalimbali ya ftari kwa ajili ya mfungo .
ntakuwa naweka post za mapisi na recipies zake kupitia humu.
karibuuni sana.




Monday 30 July 2012

RAMADHAN KAREEM WADAU

Tukiwa tunaendelea vyema na mfungo wa m,wezi mtukufu wa ramadhani ikiwemo leo tunamalizia kumi la kwanza inshaalah ,
nawatakia mfungo mwema wa ramadhan tujitahidi kufanya ibada ktk mwezi huu ili Mmungu atusamehe madhambi yetu .
Ramadhan Kareem.