Tuesday 31 July 2012

MAPISHI YA VIBIBI


 MAHITAJI

1.Mchele Vikombe 2 
2. Tui la nazi  Kikombe 1 na nusu
3. Mafuta kijiko 1 cha chakula
4. Hamira Vijiko vya chai   2
5. Unga wa ngano kijiko 1 cha chakula
6. Hiliki  kiasi upendavyo
7. Sukari  Kikombe 1
JINSI YA KUANDAA 

1·  Osha na roweka mchele usiku mzima ndani ya maji baridi.
2·  Mimina vifaa vyote isipokuwa sukari , ndani ya mashine ya kusagia (blender) na usage mpaka mchele uwe laini.
3·  Mimina ndani ya bakuli na ufinike , kisha weka pahali penye joto ili mchanganyiko ufure.
4·  Ukishafura , mimina sukari na changanya vizuri ; ukiona mchanganyiko ni mzito sana, ongeza maziwa kidogo.
5·  Weka chuma kipate moto.
  Paka mafuta au samli kidogo kwenye chuma kisha mimina mchanganyiko kiasi kuunda duara na ufunike.
  Utazame ikishaiva upande mmoja , geuza upande wa pili mpaka iwe tayari.
  Endelea Mpaka umalize mchanganyiko wote,panga kwenye sahani na tayari kuliwa.
VIBIBI KATIKA PICHA.
 ENJOY YOUR MEAL

No comments:

Post a Comment