Tuesday 31 July 2012

PISHI LA KATLES

MAHITAJI

1. Viazi Ulaya  Nusu Kilo
2. Kitunguu swaum Kikubwa 1
3. Myama ya kusaga Robo 
4.Limao
5.Vitunguu Maji Vikubwa 3
6. PiliPili Manga 
7. PiliPili mbuzi
8. Mayai 2
9. Mafuta kiasi
10. chumvi.
11.unga wa ngano kikombe 1

JINSI YA KUANDAA

menya viazi vyako na uvioshe vizuri kwa maji safi
weka kwenye sufuria na uweke chumvi kiasi 
weka jikoni vichemke hadi viwe laini .
wakati viazi viko jikoni andaa nyama yako ya kusaga 
weka chumvi,ndimu,swaum,tangawizi,na pilipili manga,na km utapenda kuweka pilipili mbuzi 
katiakatia vitunguu maji  na uweke jikoni nyama nayo iwive.
viazi vikiwa tayari mwaga maji na uhakikishe hamna maji na uanze kuviponda hadi madonge yaishe.
nyama ikiwa tayari epua na uweke pembeni ipoe.
weka ndimu ktk viazi vilivyopondwa pamoja na pilipili manga kiasi changanya kwa pamoja.
tengeneza shape ya duara ukiweka kishimo kati kwa ajili ya kuweka nyama ya kusaga.
tengeneza madonge yako huku ukiweka nyama kati na kufunga kwa kutumia viazi vilivyopondwa.
baada ya kumaliza madonge yote .
andaa mayai kwenye kibakuli na uyachanganye alafu weka chumvi.
weka mafuta jikoni yachemke
then chukua donge moja moja zamisha kwa unga wa ngano (husaidia kutokuvurugika) halafu dumbukiza kwa mchanganyiko wako wa mayai na uweke kwenye mafuta.
kaanga hadi vibadilike rangi ,
katlesi zako ziko tayari kwa kuliwa..
na katlesi zako zitakuwa hivi katika picha.


ENJOY YOUR MEAL.

No comments:

Post a Comment