Monday 19 January 2015

AMBER ROSE AENDELEA KUBREAK THE INTERNET MITANDAONI.





Mwanamitindo maarufu nchini Marekani aendelea kubreak the internet kwa kutupia picha zake akiwa na vivazi matata sana..
Amber Rose mwenye umri wa miaka 31 na ni mama wa mtoto mmoja ambaye alizaa na aliyekua mume wake Wiz Khalifa..

Haya wale wabongo wa kubreak the internet mupo...
Ya walimwengu...

Friday 16 January 2015

UTUNZAJI NA UREMBO WA MIDOMO/LIPS

Tukirudi kwenye safu yetu ya urembo, leo tujue jinsi gani ya kuremba mdomo yako na kuweza kuifanya yenye mvuto zaidi kwa wanaokutazama.

midomo ni sehemu muhimu sana katika kukamilisha unadhifu na muonekano mzuri
Ngozi ya midomo ni laini sana na inahitaji uangalizi katika kuitunza na kuifanya iwe mizuri zaidi.

utunzaji wake wala hauhitaji mambo mengi sana ni kidogo tuu.

Epuka kuacha midomo ikawa mikavu kwa mda mrefu kwani inasababisha kukatika na kuweka gamba gumu kwa juu.
hvyo jitahidi kutumia mafuta laini ya midomo/ vaselline / ama mafuta mengine mazuri ya mgando ambayo yanafaa kulainisha midomo yako.

vilainishi hivo nlivotaja hapo juu vitasaidia kulainisha midomo yako na kuifanya iwe na afya njema na sio yenye kukauka.

zoezi la upakaji wa vilainishi hvyo linashauriwa liwe , usiku wakati wa kulala paka mafuta yako mdomoni inasaidia kuamka ukiwa na lipsi laini na nzuri na pia akti wowote ambao utahisi lipsi zako zimekauka unatakiwa upake vilianishi hivi.

then ukipaka vilainishi ndio utaweza rembesha midomo yako kwa lipstick mbalimbali kutegemeana na skin tone yako au rangi ambayo umependezewa kuipaka siku hiyo.




JINSI YA KUPAKA LIPSTICK

  • Anza kwa kupaka kilainishi kabla ya kupaka lipstick yako. LipBalm
  • Paka Lip Liner ya colour ya lipstick ambayo unatarajia kupaka au kwa colour yeyote utakayopendezewa nayo.
  • Chukua lipstick yako pakaa ukianzia lips za chini ukifuatiwa na za juu na kuichanganya vizuri.
  • Kama unapendelea mg'ao zaidi unaweza kupaka lipshine kwa juu kung'arisha midomo yako.
  • Baada ya kufata steps hizo hapo, utakuwa umekamilisha upakaji mzuri wa Lipstick katika midomo yako na kuifanya ya kuvutia.

ZINGATIO

Angalia sana lipstick unayopaka na rangi ya ngozi yako. kwani kunalipstic nyingine zinachagua rangi ya ngozi.

Kwa mahitaji ya lipstick, lipliner, wanja , poda wasiliana nasi kupitia no 0716 666640. instagram @kithuraah.
karibuni wote.

Tuesday 13 January 2015

HAYAWI HAYAWI KIMIMBA NDWII, CHIBU JNR YUKO NJIANI

Baba na Mama Kijachooo, wale wenye kutaka malimaoo wanicheck niwaleteeee......

Papa Chibu Dangote ak.a Diamond Platinums hatimaye anatarajia kupata mtoto toka kwa The BossyLady herSelf ZARI.

Hii imethibitika baada ya jana Diamond Platinumz kupost Picture ya Utrasound ya kibebi hicho katika page yake ya Instagram akisema kwamba.. napost hyo haikukaa mda mrefu Diamond akaidelete faster, kumbe maskini alishachelewa wadaku wakawa tayari washaidaka, chezea wadaku wa kujitegemea wewe, yani 24/7 wanafatialia A to Z ya kinachojiri katika page yako ..lol tisha sana wadaku...

'' i can not wait to have you in my hand. Chibu_Jnr''


mi binafsi ningekua mshauri wa Diamond na Zari, ningewashauri wangekausha kwanza hadi mambo yakwive yani si unajua pembe la ng'ombe halifichiki eeh basi wangefanya kutusuprise aiseee..
haya all in all tunawatakia kila la kheri katika malezi ya kijacho hicho ,isije kua kama stori za Penny enzi zileeeeeeeeeeeee......

Thursday 8 January 2015

STORI KATIKA PICHA KUHUSU DIAMOND NA ZARI. PART ONE..

1.Ilianzia kwenye ndege kuja Dar, ilikua kama project 
Selfie za kwenye ndege Pjoect

Project ikaanza

Project ikaendelea

wakakiss hivi,project ikiwa inaendelea
Wenyewe waka confirm kwamba ni project.
2.Ikaja siku ya kupokea tuzo za chanel O huko South Africa Zari akamsindikiza Diamond pamoja na mama mzazi
mapicha yakawa hivi

na hivi

na hivi

na hivi pia
dada Kimwana nae alikuepo South Africa
 3. ikaja mapokezi ya Diamond Uganda kwa ajili ya Zari Ciroc White Party, nayo ilikua hivi






kwenye lift kuelekea hotel ikawa hivi,
wakaamka hivi kwa ajili ya party usiku

usiku ukafika kwa ajili ya Zari Ciroc White Party ikawa hivi




Shake up ua bum bum your bum,, party party

Mwisho ikawa hivii,, kissing

STORY ITAENDELEA KESHO WADAU MANA NI NDEFU HADI ILIPOFIKIA SASA, NA PICS ZILIZOWEKWA NI CHACHE NIMECHKUA MAALUM TUU ILI KUNOGESHA STORY..

Wednesday 7 January 2015

MISS BUMBUM 2012- BRAZIL AOZA MISULI KWA AJILI YA KUONGEZA MAKALIO


Miss Bum Bum 2012 huko nchini Brazil kwa jina la Andressa Urach amekumbwa na majanga ya kuoza misuli ya mapaja hii yote ni kwa sababu ya kuchoma sindano ya kuongeza makalio na mapaja yake kipindi cha miaka mi3 nyuma,


mrembo huyu mwenye umri wa miaka 27 alikua mwanariadha nchini humu na mwisho aliishia kwenye mashindano ya urembo.mrembo huyu alikaa wodini kwa mda wa mwezi mzima akihofia kupoteza mguu wake wa kushoto baada ya misuli kuoza na kumsababishia maumivu makali sana.
mrembo huyu aliziona picha zake zilizochukuliwa kipindi yuko mahututiambazo zilionyesha jinsi alivotobolewa tobolewa na kubandikwa plasta.

Miongoni mwa surgery ambazo amewahi fanya mrembo huy ni pamoja na , kuongeza matiti, kunyoosha pua, kupunguza mashavu ya shehemu za siri na nk.
Imethibitika kuwa Brazili ni moja ya nchii inayoongoza kwa watu wengi walio fanyiwa upasuaji wa mwili(Plastic Surgery).
mrembo huyu ameonesha kuwaogopesha wengi kutokana na madhara aliyoyapata kwa ajili ya upasuaji uliofanywa kwenye mwili wake.

Haya wale warembo wetu mnaopenda urembo kupitiliza kushinda jinsi alivokupanga MwenyeziMungu na kuongezea vya kuongeza haya ndio madhara yake sasa so just be natural jamani nini tena unaongeza ili iweje sasa kwa mfanoo.. na haya ndio matokeo yake sasa..