Monday 29 July 2013

NANDO ARUDI NYUMBANI .



hasira hasara ,yamemkuta mshiriki toka Tanzania ndani ya jumba la Big Brother Nando baada ya kukubuhu kurudia makosa ambayo alishapewa onyo na ni baada ya kutaka kuzipiga na mhiriki mwenzie Elikeem.

nando alisikika akimtupia matusi mshiriki mwenzie huyo na kumtishia kumuua ,hilo la kutaka kumuua lilithibitika pale alipokuwa akionekana na kisu ambacho inasadikika alikua anasubiri kinuke ili picha lianze (thinking) ambacho alikua analala nacho chini ya mto wake ,,,weeeh nando weeh umetoa wapii hii mbona waTz tunakukubali then umeharibu sasa..

Bigie alimuita Nando na kumhorodheshea makosa yake ambayo alikua akiyafanya ,ambayo yalikua ni nje ya masharti ya mjengoni hapo ,na hapo hapo akatamka kuwa huo ndio ulikua mwisho wa mchezo huo kwake .nakukosa kabisa kupata chance hata ya kuagana na washirii wenzie ndani ya jumba hilo .

POLE SANA NANDO NA KARIBU SANA NYUMBANI .

 

No comments:

Post a Comment