Wednesday 9 July 2014

10.07 KUMBUKUMBU YA MIAKA 12 YA BABA YANGU AMIRI HUSSEIN KAUMO



siku kama ya leo 10.07.2002, ni siku ya majonzi sana kwangu kwani ndio siku baba yangu kipenzi Mr. AMIRI HUSSEIN KAUMO alifariki ,ni miaka 12 sasa tangu tupatwe na msiba huu , naimani huko uliko uko pahala pema.ulikua Baba mzuri, rafiki mzuri sana kwangu ukiniongoza vyema ktk kipindi chote cha uhai wako,ukinifunza mengi mengi na kusisistiza zaidi kwenye elimu. kwa hilo nasema Ahsante sana.

nnamengi ya kusema lkn naomba niseseme mengi zaidi, nakupenda baba yangu na utaendelea kuwepo katika mawazo,akili na moyo wangu kila siku za maisha yangu. nakuombea salama huko uliko, Mmungu akupe kauli njema huko uliko, akupunguzie adhabu , akuweke mahala pazuri kwani hata mimi nakuombea salama huko uliko Baba yangu .

nakukumbuka sana, natamani ungekua nami hadi leo hii ukaona jitihada zangu katika kutafuta na imani hata huko uliko unaona na unajivunia kwa njia moja au nyingine ..
namshukuru Mmungu kwa kipindi chote hichi nimekua na afya njema na kila kitu kinaendelea sina budi kusema ""alhamdulillah""

MMUNGU AKULAZE MAHALA PEPA PEPONI BABA YANGU AMIRI HUSSEIN KAUMO


No comments:

Post a Comment