Wednesday 11 April 2012

LULU APANDISHWA KIZIMBANI KWA SIRI


Elizabeth Michael (Lulu) leo amepandishwa
kizimbani katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam na
kusomewa shitaka la mauaji.
Lulu alipandishwa kizimbani kwa usiri akitokea Kituo cha Polisi cha
Oysterbay alikokuwa akishikiliwa na
kupandishwa kizimbani moja kwa moja bila
kuwekwa mahabusu
kama iwavyo kwa washitakiwa wengine
wanaosubiri kusomewa kesi zao.
Baada ya kupandishwa kizambani
alisomewa shitaka lake na Mwendesha
Mashtaka Mkuu wa Mahakama hiyo,
Elizabeth Kaganda ambapo alisema Mnamo
Aprili 7 mwaka huu majira ya saa saba za
usiku maeneo ya Sinza Vatican jijini Dar es
Salaam Elizabeth Michael (18) alimuua
Steven Kanumba. Katika kesi hiyo
mshitakiwa hakutakiwa kujibu lolote
isipokuwa alinyoosha kidole na kupinga
umri uliotajwa kuwa ana miaka 18 na
kusema umri wake ni miaka 17. Baada ya
kusomewa shitaka hilo, Lulu alipelekwa
gerezani Segerea na kesi yake itasikilizwa
tena aprili 23/2012

No comments:

Post a Comment