Saturday 22 June 2013

MIMBA YA PENNY WA DIAMOND PLATINUMZ YATOKA



TAARIFA ya ndani zinazodai kwamba, mimba ya mchumba wa Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nassibu Abdul ‘Diamond’, Peniel Mgilwa ‘Penny’ imechoropoka zimevuja na Risasi Jumamosi imezinasa.

Kwa mujibu wa chanzo makini kilichojitambulisha kwa jina la wifi (jina kapuni) kwa Penny, ni kwamba mtangazaji huyo wa Runinga ya Channel 10 cha jijini Dar hivi sasa hana ujauzito tena kama wengi wanavyodhani.
“Penny hana mimba jamani, yupo fiti kabisa na sidhani hata kama anatarajia kushika ujauzito leo wala kesho,” kilisema chanzo hicho.

Hata hivyo, wifi huyo alisema kwamba awali kulikuwa na dalili zilizoonesha kwamba Penny alikuwa ni mjamzito kutokana na mtangazaji huyo kutumia vitu vichachu kama vile maembe na mara kwa mara alikuwa akiumwa hadi kufikia kulazwa hospitali.
Inadaiwa kwamba Penny alipotoka hospitali alionekana kuwa fiti zaidi na hakuwa na dalili zozote za kuwa na ujauzito kama ilivyokuwa siku za nyuma.
Baada ya gazeti hili kupata habari hizo lililimpigia simu Penny ili kuthibitisha madai hayo:
Risasi Jumamosi: Mambo vipi, Penny pole sana.
Penny: Pole ya nini sasa?
Risasi Jumamosi: Si nimesikia kwamba unaumwa jamani na ukakumbwa na mkasa mwingine?
Penny: Mkasa gani huo unaousema maana mimi niko fiti tu.
Risasi Jumamosi: Nilisikia kwamba baada ya kuumwa na kulazwa hopsitali mimba yako ikatoka?
Penny: (Kimya kwa dakika 3) Asante ni mipango ya Mungu.
Risasi Jumamosi: Sasa unatarajia lini utapata tena mimba nyingine?
Penny :(Kwachuuuuuu). Simu ilikatwa na hata ilipokuwa ikipigwa tena haikuwa ikipokelewa.

chanzo: globalpublishers.info

WEMA NA KAJALA KIMENUKA



Utabiri wa wengi kuwa ushosti wa waigizaji masistaduu wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu na Kajala Masanja kutumbukia nyongo unadaiwa kutimia na sasa wametibuana,

Habari za ndani kutoka kwa mtu wa karibu (jina linahifadhiwa), mwanzoni baada ya Wema kumlipia Kajala faini ya Sh. milioni 13 na kumnusuru kutokwenda Segerea a.k.a Segedansi, wawili hao walikuwa marafiki kama pete na kidole.


“Walishinda wote, walilala wote, walikwenda klabu wote yaani Kajala alikuwa anamnyenyekea ‘madam’ Wema kwa kumuepusha na kifungo cha miaka 7 jela,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:

“Kuna wakati hapa katikati Kajala alikuwa kama katibu muhtasi wa madam, si unajua lazima atumikie fedha za watu?
“Kabla hajaenda Mwanza kwa ajili ya mapumziko kwa bibi zake, nilimsikia Kajala akilalama kuwa madam aliamka siku moja akawa amemchunia, unaambiwa hata salamu ikawa hakuna.

“Hapo ndipo maneno ya pembeni yakaanza kwa sababu mbali na Kajala, Wema pia ana wapambe wengine na mbali na Wema, Kajala naye ana kampani. Kwa hiyo sosi ya manenomaneno ni hizo kampani zao.

“Ipo siku kabisa Wema alimlalamikia Kajala hadharani kuwa amekuwa akimsema vibaya kwa watu.

“Yale maneno yalimuuma sana Kajala, ikabidi arudi nyumbani kwao lakini akawa anaogopa kumwambia mama yake kuwa ametibuana na Wema hadi alipotimkia Mwanza.

“Lakini kabla ya hii ishu ya kulaumiana, kipindi cha nyuma kidogo Kajala alipata dili la kwenda kurekodi filamu nchini China na mastaa wengine lakini ikadaiwa kuwa Wema alichomoa hivyo mwigizaji huyo hakwenda pamoja na kwamba alishapewa baraka zote na baba yake.

“Unaambiwa alikuwa amekamilisha taratibu zote za kwenda China, hadi tiketi alikuwa ameshakata lakini suala hilo lilipotua kwa Wema, ilidaiwa kuwa alikataa kumruhusu.


TATIZO MILIONI 13?
“Mimi nakwambia zile milioni 13 zinamkosesha raha Kajala hadi unamuona kabisa kwamba ana stress (msongo wa mawazo).

“Wewe fikiria, kazi inayomwingizia mkwanja ni filamu, sasa unaambiwa inadaiwa kuwa madam hataki acheze filamu za watu wengine, sasa ataishije jamani?

“Mimi nakwambia ndiyo maana ameamua kwenda kupumzika Mwanza baada ya kuwa wananuniana kwa kwenda mbele.”


Baada ya kupata habari hizo, mwandishi wetu alimtafuta Wema kwa njia ya kilongalonga chake cha kiganjani ili kupata undani wa sakata hilo lakini hakupatikana hewani.

Baadaye mwanahabari wetu alisaga lami hadi kwa staa huyo Kijitonyama, Dar, alipogonga geti alitoka mlinzi aliyedai kuwa ‘malkia’ alikuwa ndani amelala na hakuhitaji usumbufu pamoja na kwamba ilikuwa saa 6:30 mchana.



Hata hivyo, mwanahabari wetu alibisha hodi ofisini kwa Wema, Mwananyamala-Komakoma ili kuzungumza na meneja wake, Martin Kadinda ambaye alikuwa na haya ya kusema:


“Ni kweli Kajala yupo Mwanza, aliomba ruhusa ya kwenda kupumzika tukampa. Hayo mengine ya kutibuana na madam siwezi kuyasemea kwa sababu yapo nje ya uwezo wangu.

“Lingekuwa ni suala la kazi hapo sawa lakini ni vizuri ukazungumza na mkurugenzi mwenyewe (Wema) lakini sidhani kama ataweza kuzungumza kwa sababu alikuwa anaumwa, amezidiwa na kupelekwa hospitali.”

Alipoulizwa Wema anaumwa nini, Kadinda alifunguka: “Sijajua lakini ugonjwa ni siri kati ya mhusika na daktari, cha msingi wewe ujue tu anaumwa.”

Baada ya kupita kote huko kusaka undani wa sakata hilo, mwandishi alimgeukia Kajala kwa njia ya simu ya mkononi akiwa jijini Mwanza na kumuuliza kulikoni kutibuana na Wema.


Huku sauti ikiwa chini, Kajala alisema: “Ni kweli kuna hali ambayo hata mimi mwenyewe nashindwa kuelewa lakini siwezi kuzungumzia kwa leo nikiamini yatapita.”

Je !haya kweli yatapita au yatakua yaleyale ya Wema na Snura mama wa majanga?
na Je ile kama hayatapita Je Kajala alichora tatoo ya jina la WEMA kama shukurani yake kwa kumuepusha na kifungo cha miaka 7 jela ataifuta au atafanyaje ,kuwa nami nikupatie habari..

kithuraah wa kaumo

Saturday 15 June 2013

HIVI NDIVYO JIDE a.k.a KOMANDO ALIVOFUNGA BARABARA NDANI YA NYUMBANI LOUNGE

HAPO WATU WAKIWA KWENYE FOLENI YA KUINGIA NDANI

TASWIRA YA NDANI KULIVOKUA

MH SUGU AKISABABISHA HAJAACHA KIPAJI CHAKE

MACHOZI BAAND

ANACCONDA MWENYEWE HUYU AKIDHIHIRIHA UANACCONDA WAKE
 

DJ CHOKA AKIFANYA MAMBO YAKE

HAO SASA ,,HADI RAHA

BONGO MUVIE HAWAKUKOSA

TEAM ANACCONDA HIYO
 

Thursday 13 June 2013

MSANII WA BONGO FLEVA LANGA AFARIKI DUNIA

Habari zilizonifikia sasa hivi punde kutoka kwa

ndugu wa karibu wa Langa zinasema ndugu yao

Langa amefariki katika hosp kuu ya Muhimbili

kwa kuumwa Malaria. Habari kamili zitawajia kwa

jinsi nitakavyokuwa napewa updates.

MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA

PEPONI.





source:DJ Choka





Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.

Thursday 6 June 2013

MUME WA MALKIA WA TAARABU BI KHADIJA KOPA AFARIKI DUNIA

Mume wa Malkia wa Mipasho Afrika

Mashariki, Khadija Omar Kopa, aitwaye

Jaffari Ally amefariki dunia usiku wa

kuamkia leo. Marehemu alikuwa

anasumbuliwa na matatizo katika

mfumo wa upumuaji na mpaka mauti

yanamfika alikuwa amelazwa katika

hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali

pema peponi.

AMEN





Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.

MTANZANIA AKAMATWA NA MADAWA NCHINI MISRI

Mtanzania FATMA a.k.a BROWN BERRY  mkazi wa ilala Dar es Salaam.
amekamatwa nchini misri akijaribu kusafirisha madawa ya kulevya kwa kutumia begi alimoweka nguo zake.
hii ni video ya jinsi maafisa wa misri walivyomkamata.
Bado haijathibitishwa kama ni kweli amehukumiwa kunyongwa tutaendelea kupeana updates kupitia hapa.
Hizi ni baadhi ya picture za mwanadada huyo .


fatma akiwa na mwanaye
 
fatma akiwa katika pozi
 
fatma akiwa na mpenzi wake
 
fatma akionekana siku aliyokamatwa na madawa yuko chini ya ulinzi
NB: WATANZANIA WENZANGU ,DADA ZANGU NA KAKA ZANGU MAISHA SIO RAHISI KIASI CHA KUJISACRIFICE ,TUJIFUNZE KUTAFUTA PESA KWA NJIA ZA HALALI NA KWA JASHO LETU ,SIO KUTAKA PESA NYINGI KWA PUPAMATOKEO YAKE NI KAMA YALOMKUTA MDADA HUYU HUKO NCHINI MISRI..INASIKITISHA SANA.
 
KAKA ZETU ,DADA ZETU WANATEKETEA KWA AJILI YA MATUMIZI YA MADAWA YA KULEVYA HIVYO BASI TUSHINDANE ILI KUEPUKANA NA HILI.

Tuesday 4 June 2013

WATANZANIA WAFURIKA KUPOKEA MWILI WA ALBERT MANGWEA

watanzania wafurika uwanja wa ndege Dar es Salaam kuupokea mwili wa aliyekua msanii wa Bongo Fleva Albert Mangwea.
 
WATANZANIA WALIOFIKA KUUPOKEA MWILI WA ALBERT MANGWEA

MCHIZI MOX AKIWA AMESHIKILIA MSALABA.
 

Add caption

BAADHI YA WASANII NA MASHABIKI WA MAREHEMU






RATIBA KAMILI YA KUPOKEA NA KUUGA MWILI WA ALBERT MANGWEA

Wanakamati wa mazishi pamoja na wasanii akiwepo Profesa Jay, Lady Jaydee, Fid Q, Stamina, Juma Nature na wengine wengi wanaelekea uwanja wa ndege kutoka Viwanja vya Leaders tayari kuupokea mwili wa Albert Mangwea

  •  mwili utawasili mchana huu.
  • baada ya mwili kuwasili uwanja wa ndege , utapelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo utapokelewa na Kuhifadhiwa.
  • baada ya mwili kuhifadhiwa waombolezaji wataelekea viwanja vya leaders kwa ajili ya maombolezo.
  •  
  • kesho saa 2 asubuhi mwili utakuwa Viwanja vya Leaders kwa ajili ya ndugu , jamaa, na marafiki kutoa heshima zao za mika mwisho hadi mnamo saa6 mchana.
  •  
  • kesho hiyo hiyo sa 6 mchana mwili utasafirishwa kuelekea mkoani kwa  ajili ya taratibu za kuuhifadhi katika nyumba ya milele.
 
MAY HIS SOUL REST IN PEACE ALBERT MANGWEA.



MWILI WA ALBERT MANGWEA WATARAJIA KUFIKA TANZANIA MCHANA WA LEO



 
 
 
 
TOKA huu msiba umetokea kumekua na habari ambazo zinaandikwa au kuripotiwa lakini hazina usahihi, pia habari ya kusafirishwa kwa mwili I mean zikwa tofauti tofauti kwenye vyombo mbali mbali lakini uhakika ni kwamba mwili wa Marehemu umepelekwa Airport ya Johannesburg June 3 2013 ambapo utasafirishwa June 4 kuelekea Dar es salaam na kufika mchana saa nane.

Hizi picha zimepigwa makusudi ili kutoa ushahidi kwa wale ambao bado walikua hawaamini kama mwili huu umefikia kwenye hatua za kusafirishwa kutokana na kuahirishwa kusafirishwa mara mbili kwa sababu ya taratibu za Serikali ya Afrika Kusini ambazo ilikua ni lazima zifatwe hasa ikizingatiwa kwamba Marehemu ni kutoka nje ya nchi hii na kifo chake ni cha ghafla.

Source: Millard Ayo

WATANZANIA WALIOKO SOUTH WAUAGA MWILI WA ALBERT MANGWEA


Watanzania waliopo Afrika Kusini wamefanikiwa vyema kutoa salam zao za mwisho kwa mpendwa wetu Albert Mangwea.

Mwili wa ngwea unatarajiwa kuingia tanzania mnamo saa 8 mchana kwa ajili ya kumpumzisha katika makazi yake ya milele.
 
JENEZA LILILOWEKWA MWILI WA ALBERT MANGWEA

WATANZANIA NA MARAFIKI WENGINE SOUTH AFRICA WAKIAGA MWILI WA ALBERT MANGWEA

KINJEKITILE AKIWA NA WATANZANIA WALIOHUDHURIA KTK KUMUAGA NGWEAR



KINJEKITILE NA WATANZANIA WENGINE WAKIBEBA JENEZA LA ALBERT MANGWEA





Monday 3 June 2013

RAMBI RAMBI ZA MSIBA WA NGWEA YAFIKIA MIL32

Mwenyekiti wa Kamati ya Msiba wa Albert Bwn: Adam Juma


KAMATI ya Mazishi ya aliyekuwa Msanii wa Bongo Fleva, Albert Mangwea ‘Ngwea’, mpaka jana mchana ilikuwa imekusanya jumla ya Sh milioni 32 kutoka kwa wadau mbalimbali.
Kamati hiyo inahitaji Sh milioni 50 kwa ajili ya kusaidia kusafirisha mwili wa marehemu kutoka Afrika Kusini mpaka Morogoro kwa ajili ya mazishi. Fedha hizo pia zinahitajika kwa ajili ya kuratibu shughuli nzima ya mazishi.
Mangwea alifariki dunia Jumanne iliyopita nchini Afrika Kusini akiwa usingizini kwa madai ya kuzidisha matumizi ya madawa ya kulevya. Alitarajiwa kuwasili nchini jana lakini kushindwa kutoka kwa ripoti ya uchunguzi wa madaktari kwa wakati, kumesababisha isijulikane atatua lini, licha ya kudaiwa kuwa anaweza kutua leo.
Kamati ya Mazishi bado inaendelea na mchakato wa kuratibu shughuli hiyo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Championi Jumatatu akiwa Mbezi Goig jijini Dar ambako ndiko kwenye msiba huo, mmoja wa waweka hazina wa kamati hiyo, Paul Matthysse ‘P-Funk’, alisema mpaka sasa kamati yake imefikisha Sh 32,259,000 ingawa wanatarajia kuendelea kupokea michango mbalimbali kutoka kwa wadau.
Miongoni mwa watu wa kwanza kutoa michango yao katika msiba huo ni P-Funk aliyetoa Sh milioni tano, Clouds Media Group (Sh milioni tano) na Push Mobile (Sh milioni tano). Juzi Kampuni ya Global Publishers ilitoa Sh milioni moja.
“Nawasisitiza Watanzania waendelee kutoa michango yao kwa ndugu yao ili kuonyesha umoja tulionao. Fedha zikiwa nyingi tunataka kumfanyia kitu mama yake ili kuendelea kumfariji kwani kipindi hiki ni kigumu kwake,” alisema P-Funk.
Wakati huohuo, wakati tunakwenda mitamboni jana, taarifa zilisema mama mzazi wa Mangwea aishie Morogoro, Denisia Mangwea, alipandwa na presha baada ya jana kupata taarifa kuwa mwili wa mwanaye umezuia Afrika Kusini kutokana na uchunguzi wa madawa ya kulevya. Alikimbizwa hospitali na inadaiwa anaendelea vizuri.
Mangwea aliwahi kutamba na nyimbo kadhaa kali zikiwemo Gheto Langu, She Got a Gwan, Mikasi na Tupo Juu.

CHANZO : www.globalpublishers.info

BALOZI WA TANZANIA AFRICA KUSINI AFIKA MSIBANI KUTOA RAMBIRAMBI ZAKE

Blozi wa Tanzania S.A akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa baba mdogo wa mangwea mbezi beach jana

akiwa na mama ake mdogo marehemu Albert Mangwea Mbezi Dar es Salaam 

Mwenyekiti wa Kamati ya msiba akisalimiana na Balozi.
 Chanzo :Global Publishers