Friday 24 October 2014

MISS TANZANIA NO3 AFUNGUKA KUHUSIANA NA USHINDI WA SITTI


Gumzo mtaani kwa sasa kwenye ulimwengu wa urembo ni ushindi wa mwanadada Sitti Abbas Mtevu ambaye hivi karibuni aliibuka mshindi katika Shindano la Miss Tanzania 2014. Tutakumbuka baada ya Sitti kutangazwa mshindi, maneno yalikuwa mengi, mara alipendelewa, mara alidanganya umri, wengine wakasema eti ana mtoto.


Yameongelewa mengi na kimsingi mpaka sasa bado ushindi wake unaonekana kuwa na makengeza. Kutokana na hali hiyo, waandishi wetu walifanya mazungumzo na baadhi ya wadau lakini kati yao alikuwa mmoja wa washiriki ambaye alichukua nafasi ya tatu, huyu ni Jihan Dimachk.
Kwenye fainali za mashindano hayo mrembo huyu alichukua Taji la Miss Tanzania Top Model 2014 na sasa fuatilia exclusive enterview hii iliyofanyika kati yake na Ijumaa ndani ya Hoteli ya Regency iliyopo Mikocheni, Dar.
Ijumaa: Habari yako Jihan, sisi ni waandishi kutoka Gazeti la Ijumaa.
Jihan: Okey, nashukuru kuwafahamu, karibuni.
Ijumaa: Tuanze na matokeo ya kinyang’anyiro cha Miss Tanzania mwaka huu, unadhani wewe ulistahili kuchukua nafasi ya tatu na Sitti Mtemvu kuibuka kidedea?
Jihan: Siwezi kuongea sana jamani lakini kwa kifupi nilikuwa nikiamini nitashinda, niseme tu kwamba it was unfair but I can’t explain (haikuwa sawa ila siwezi kuelezea).
Ijumaa: Kwa nini unasema hivyo? hebu fafanua kauli yako.
Jihan: Sipendi kuwa muongeaji sana, naheshimu maamuzi ya majaji na Kamati ya Miss Tanzania lakini ukweli uliopo moyoni mwangu ni kwamba nilijiamini na ndiyo maana niliingia kwenye kinyang’anyiro nikijua ushindi ni haki yangu.
Ijumaa: Wapo wanaosema ulikuwa na kila kigezo cha kuwa Miss Tanzania 2014 lakini umetoswa kutokana na rangi yako ukihisiwa wewe si Mtanzania, unaliongeleaje hili?
Jihan: Sipendi kabisa kusikia maneno hayo, mimi ni Mtanzania, nimezaliwa Mwanza, mama yangu ni Msukuma na baba yangu Mlebanon. Tangu naingia kwenye shindano hili waandaaji walinihoji, wakafuatilia hilo na kutambua ni Mtanzania, ingekuwa tofauti sidhani kama ningeruhusiwa kushiriki.
 Ijumaa: Kwa mfano ikitokea Sitti akavuliwa taji kutokana na haya yanayozungumzwa, uko tayari uvishwe wewe?
Jihan: Siwezi kulijibu swali hilo kwani haijatokea. Endapo itatokea na waandaaji wakanifuata kuniambia hivyo, hapo ndiyo nitakuwa na la kuzungumza.
Ijumaa: Unamuongeleaje Sitti Mtemvu?
Jihan: Kwa sababu ndiye aliyevishwa taji, naheshimu ushindi wake, namkubali kuwa ni mrembo na siwezi kupingana na maamuzi yaliyotolewa.
Ijumaa: Umechukua nafasi ya tatu ambayo nayo si haba, una mipango gani ya baadaye?
Jihan: Nina mambo mengi ya kufanya. Nina ndoto za kuwasaidia wanawake na watoto lakini pia nahisi nina jukumu la kusaidia katika suala la elimu nchini, nitajipanga kufanikisha hayo.
Ijumaa: Kwa nini elimu?
Jihan: Nimekuwa nikikutana na watu wengi ambao elimu imekuwa kikwazo kwenye maisha yao, nikawa nimejiapiza kuhakikisha nawasaidia kadiri nitakavyoweza.
Ijumaa: Asante sana Jihan, tunakutakia mafanikio katika yale unayopanga kuyafanya.
 Jihan: Nashukuru sana.

SOURCE: www.globalpublishers.info

Wednesday 22 October 2014

DADA WA KAZI ATEKETEZA NYUMBA SABABU YA JIKO LA GESI

Huko maeneo ya kigamboni , nyumba yateketea kwa moto chanzo ni jiko la gesi.
mwenye nyumba hiyo ambaye jina halikupatikana mfanyakazi wa ECO BANK.
Anayesadikiwa kua Mwenye nyumba hiyo
chanzo cha moto huo inasemekana ni jiko la gesi ambapo mfanyakazi wa ndani aliweka maharage na kutoka nje ya nyumba huku akiacha jiko likiwa linafanya kazi bila uangalizi wa mtu yeyote.\
bahati nzuri ni kwamba watoto walikua shuleni na wazazi walikua kazini wkati tukio hilo linatokea.










Tuweni makini sana na wadada wa kazi ,ikiwezekana wapewe mafunzo ya jinsi ya kutumia vitu vya ndani especially majiko ya gesi, na uangalizi mzuri wa nyumba kwa jumla.
Wadada wa kazi na nyie muwe na huruma jamani maana hii ni hasara kubwa sna kwa mabosi zenu,kwanini hamtuliii khaa! ngachokaaa..

Tuesday 21 October 2014

MAHOJIANO YA MWANDAAJI WA MISS TANZANIA NA WAANDISHI WA HABARI


Mwaka 2005 kulikua na ushindani kidogo, mwaka 2006 kulikua na ushindani  wa Wema na Jokate na upinzani huu umeendelea kuwepo kwenye mashindano yetu lakini ya mwaka huu imezidi mno, kumekua na matusi… kashfa na hata naona wamevuka mpaka na kuingiza mambo ya kisiasa ambayo sisi hatuyapendi, huu ni mchezo kama mchezo mwingine wowote… yani taji la mwaka mmoja limefunika mpaka katiba na Simba na Yanga?
Hayo ni maelezo aliyoyatoa Mr. Hasheem Lundenga mbele ya Waandishi wa habari Dar es salaam October 21 2014 kuhusu ishu ya Miss Tanzania ambae aliandikwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mrembo huyu kudanganya umri, elimu na mambo mengine.

Yafuatayo ni mambo waliyoyasema Hasheem Lundenga na Miss Tanzania Sitti.
‘Walidai kwamba Miss Tanzania ana mtoto baada ya kutoka picha moja akiwa na mtoto, nasema katika utafiti wetu sisi Miss Tanzania hana mtoto na mwenye vithibitisho halali kwamba ana mtoto atuletee, kama kuna uthibitisho wa cheti cha kuzaliwa cha mtoto….. leta hicho cheti’ – Lundenga
‘Hili la sisi kuchukua rushwa kutoka kwa baba wa Sitti, Abbas Mtemvu…. jamani hii ni stori ya kijingajinga, ni mambo ya kipumbavu sana kuandika haya mambo, hamjui taratibu zetu tunavyowapata majaji na wanavyofanya kazi…Majaji huwa wanatafutwa siku nne za mwisho na huwa hakuna mtu anajua atakua Jaji na huwa tupeleka majina 15 BASATA na wao ndio wanaturudishia majina tisa ya Majaji waliopitishwa’ – Lundenga
Magazeti mbalimbali yameripoti kwamba Sitti alikua na Masters, ukweli ni kwamba katika fomu tulizonazo sisi Sitti hajaandika hata sehemu moja kwamba amesoma mpaka Masters, swala la Masters limetoka wapi? ni uongo huo’ - Lundenga
‘Kuhusu swala la yeye kuzungumza kifaransa, mtu anajua lugha ya kimataifa mbona kwenye mashindano ya dunia wanazungumza Kifaransa na lugha nyingine? lakini mbona hata kwenye fainali alijibu kwa Kiingereza pia? Kifaransa zilikua ni mbwembwe kuwashawishi Majaji, na kweli walishawishika na ndio maana akashinda’ – Lundenga
‘Jingine ambalo ni kubwa zaidi ni swala la umri lililozungumzwa sana, katika mashindano yetu washiriki wote hujaza fomu na kuandika tarehe ya kuzaliwa, fomu ya Sitti hii hapa na inaonyesha amezaliwa May 31 1991 kwa hiyo alitimiza masharti ya kushiriki kwa kuwa ana umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 24′ – Lundenga
‘Wote walioshiriki Miss Tanzania 2014 akiwemo Sitti walituletea vyeti vyao Original vya kuzaliwa tarehe 13 na kisha tukatoa nakala kupitia hivyo vyeti vyao Original’ – Lundenga
‘Sisi kazi yetu sio kupeleleza sana, tukipata information chache zinatutosha… kama mtu anatatizo na hiki cheti cha Sitti cha kuzaliwa akafanye utafiti, ukipata ukweli tuletee sisi lakini kazi ya uchunguzi sio ya kwetu’ – Lundenga
Baada ya Lundenga kuongea, Miss Tanzania 2014 Sitti nae aliongea machache kwamba ni kweli ana umri wa miaka 23 vilevile cheti chake cha kuzaliwa kilipotea sababu amekua akisafiri mara kwa mara’ -Sitti
Waandishi wa habari walipotaka awaambie na uthibitisho kama aliripoti Polisi kuhusu kupotea kwa cheti chake, Sitti alisema ‘sikutegemea haya maswali leo kwahiyo sikuja nimejiandaa kihivyo, kama mtakua mnahitaji kunihoji mnaweza kupanga siku yenu na mkanihoji’ – Sitti
Kuhusu yeye kuwa na mtoto Sitti amejibu kwa ufupi kwa kusema >>> ‘Nadhani inajieleza kama Muheshimiwa alivyosema kwamba sina mtoto na mkitaka tunaweza kwenda Hospitali kwa sababu naona kama mnaniandama kwa vitu ambavyo sio vya kweli’
Kuhusu ukweli kama hati ya kusafiria pamoja na leseni ya gari vilivyosambazwa mitandaoni ni kweli vikionyesha kwamba amezaliwa mwaka 1989, Sitti amesema ‘Sitogusia hilo swala sababu nilivyokua nakuja kuomba Miss Tanzania niliomba cheti cha kuzaliwa, hivyo vitu vingine ni maisha binafsi…. kwahiyo sidhani kama na nyie mngependa kuona mtu anachukua leseni ya gari au Passport iwe ya kweli ama feki na kuiweka kwenye mtandao’
Hayo ndio maelezo yaliyotolewa leo kwenye mkutano na Waandishi wa habari…. kama una comment yoyote iandike hapa chini na itatufikia.

mmh ya ngoswe muachie ngoswe, tulitegemea Bibi Sitti angetusuprise lkn haya ndo yalojiri.

credit to: millardayo.com

KIDS CORNER FASHION

Pata muonekano wa mtoto wako kupitia picha toka kwa wenzetu.
kufanya mtoto aonekane mrembo zaidi.
mambo ya usmart yanaanzia utotoni,yani waswahili wanasema mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
haya sasaaaaaa






Thursday 16 October 2014

THURSDAY MISHONO













kwa msaada wa fundi kwa mishono mbalimbali
wasiliana na Kithuraah Collections
Whatsapp no : 0716 666640
karibuni nyote.

MISS TANZANIA UMRI WAMUUMBUA

moja ya profile ya mtandao wa kijamii.

Mshindi wa Kinyang'anyiro cha Redd's Miss Tanzania 2014 Miss, Sitting Mtemvu azua gumzo kwa jamii baada ya kusema anaumri wa miaka 18 na katika umri huu akiwa ametunukiwa shahada ya uzamili yani masters, amezua maswali mengi Sana kwa waTanzania na kuanza kufuata hatua ya kumjua rasmi kupitia mitandao ya kijamii na imeonyesha kua miaka mi3 nyuma alikua na miaka 25 je iweje sasa anamiaka 18?
Na Je Kama ana miaka 18 alianza shule akiwa na miaka mingapi ?
Kama s/msingi miaka 7
O-level miaka 4
A-level miaka 2
Degree ya kwanza 3
Degree ya pili miaka 2
JUMLA YAKE NI MIAKA 18.........
JE AMEHESABIA UMRI ALOINGIA DARASANI TUU AMA NINII..
WASWAHILI WANASEMA UKIWA MUONGO UWE NA KUMBUKUMBUUUU..
YA WALIMWENGU HAYA.



Wednesday 15 October 2014

FAST JET MAJANGA


SHIRIKA la Ndege la Fast Jet linalotoa huduma ya usafiri wa anga katika baadhi ya mikoa ya Tanzania na nje ya nchi, limelalamikiwa na wateja wake mbalimbali kutokana na jinsi linavyofanya kazi, Risasi Jumatano lina habari kamili.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili, baadhi ya wateja hao wamesema kuwa, matangazo ya kila siku kuwa shirika hilo linatoa huduma ya usafiri wa anga kwa bei nafuu ni usanii, kwani tiketi zinazouzwa kwa bei hizo ndogo, daima huelezwa kuwa zimekwisha.
“Wanatangaza kuna tiketi za shilingi 32,000, ni uongo, mimi binafsi nimewahi kuulizia hizi tiketi mara kadhaa, lakini kila nikiomba ninaambiwa zimeisha na hata ndani ya ndege sijawahi kukutana na msafiri mwenye tiketi ya bei hizo,” alisema Samuel Kuntu, mkazi wa jijini Mwanza.
Aliongeza yeye amewahi kusafiri mara kadhaa na ndege za Fast Jet, lakini amegundua upungufu mkubwa wa shirika hilo, ikiwemo nauli kubwa tofauti na inavyotangazwa kwenye vyombo vya habari.
“Jana (Jumapili iliyopita) nilikuja na ndege hii na nimelipia shilingi laki nne kwa safari ya Dar, bei hii ni kubwa, nadhani ATCL ndilo shirika lenye bei rahisi, lakini si hawa,” alisema Kuntu ambaye alionekana kujua mengi kuhusu Fast Jet.

Alisema shirika hilo la ndege lina utaratibu unaomuumiza mteja hasa pale anapoahirisha safari au kuchelewa ndege, tofauti na mashirika mengine kama Precision Air na Air Tanzania.
“Inapotokea abiria amechelewa ndege (no-show), Fast Jet humtaka alipe tiketi nyingine na kulipa asilimia 100, wakati mashirika mengine humtoza faini abiria ambaye amechelewa ndege kwa asilimia 25 ya bei aliyonunulia tiketi kisha kumpangia siku nyingine ya safari.
“Wakati mwingine wanaahirisha safari au ndege kuchelewa lakini mteja hafidiwi kwa chochote, ila mteja akichelewa, harudishiwi hata shilingi wala kupangiwa siku nyingine, alisema mfanyabiashara huyo anayesafiri mara kwa mara kati ya Mwanza na Dar es Salaam.
Msafiri mwingine , Sunday Shomari ambaye alisafiri na ndege hiyo akitokea Arusha kwenda Dar es Salaam, alisema alisahau simu yake ya mkononi ya gharama kubwa pamoja na Ipad yake ndani ya ndege hiyo, lakini muda mchache baada ya kurejea hakupata vitu vyake.
“Nilikuwa na mke na watoto tunatoka Arusha, tulipofika Dar es Salaam tukashuka na kuvisahau vitu hivyo kwa bahati mbaya, tulipofika nje mke wangu akaniuliza simu yako ipo wapi? Nikakumbuka nimeisahau ndani ya ndege, nikarudi uwanjani na kuwaomba walinzi wanisaidie niende nikachukue simu yangu.

“Wakaniambia wao hawana mamlaka ya kuingia ndani ya ndege ile, badala yake wakanisaidia kuwaambia wafanyakazi wa ndege kuwa waniangalizie vitu vyangu pale nilipokaa, lakini jambo la ajabu eti wakadai hawakuviona, wakati mimi nilikuwa msafiri wa mwisho kushuka kwenye ndege, ina maana hakukuwa na mwingine baada ya mimi kushuka ambaye ningeweza kusema l ndiye aliyechukua vile vitu,” alisema Shomari ambaye ni mtangazaji wa zamani wa ITV na Radio One, kwa sasa anafanya kazi Sauti ya Amerika (Voa) jijini Washington, Marekani.
Abiria mwingine aliyekataa jina lake kutajwa gazetini, alisema mshangao mwingine kwenye ndege za shirika hilo ni kuuziwa vitu ambavyo katika mashirika mengine, wasafiri hupewa bure akitolea mfano soda, bia na viburudisho vingine.
Mwandishi wa habari hizi alifika katika ofisi za Fast Jet zilizopo Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutaka maelezo ya uongozi kuhusu tuhuma hizo, lakini walinzi walimzuia kuingia ndani na kutakiwa kuchukua anuani ya barua pepe ya msemaji wake, kwa maelezo kwamba ndiye angeweza kumsaidia kwa mambo ya kihabari.
Mwandishi aliandika madai yote na kuyatuma kwenye anuani hiyo akitaka kuonana na uongozi kwa ajili ya kujibu maswali kadhaa, lakini afisa uhusiano aliyejibu ujumbe huo, Lucy Mbogoro, baadaye alilitaka gazeti hili kuandika maswali hayo na kuyatuma, sambamba na nakala ya sura ya mbele ya gazeti.
Lakini hata baada ya kutuma maswali hayo kama ilivyotakiwa, Fasjet wameshindwa kutoa majibu na Lucy alipopigiwa simu na kuulizwa, alidai anayehusika na majibu hayo ametingwa na kazi.
Hata hivyo, gazeti hili bado linafuatilia kwa karibu ili kupata majibu ya maswali hayo.
CREDIT TO : GLOBAL PUBLISHERS.

Monday 13 October 2014

FACIAL MAKEUP: CONTOURING AND HIGHLIGHTING TUTORIAL


FACIAL MAKEUP/ MAKE UP YA USO 

Mahitaji
  1. Cream foundation kit 

 
kit hii ni ya foundation ambayo itakua na lighter foundation na dark/contour foundation.
zinapatikana kwa brand tofauti MAC, SLEEK and IMAN na design.

2. Brushes  & Sponge
 
brush ni kwa ajili ya kuweka contour and highligher, wakati sponge itatumika ku changanya mchanganyiko huo.

3.Cake Powder


hii itatumika baada ya kuchanganya mchanganyiko wa highlighter na contour, itapakwa juu ili kuweka sawa mchanganyiko na kupata rangi nzuri.

kwa mahitaji hayo hapo juu, hii picha itaonyesha ni wapi pa kuweka highlighter na wapi kuweka dark/contour ili kutengeneza makeup vizuri.



na kupitia video hii utapata kuona jinsi ya mchanganyiko unavyokua, kuanzia mwanzo hadi mwisho.



kwa mahitaji ya vifaa au mahitaji ya kufanya facial Makeup,check na Kithuraah Collections kupitia Whatsapp # 0716 666640.
unapata bidhaa ya uhakika na original.
Mac,Sleek, Marybellyn katika form ya powder, foundation,Makeup Kit,Brushes, Sponge Wanja na kila kitu kuhusiana na Urembo
karibuni .

KURINGARINGA KUNAVYOWAPONZA MABINTI.!!


Kuringa kwa wasichana wa kibongo ni athari za malezi. Ulaya mtoto wa kike na kiume wanakua pamoja.. wanahug, wanakiss, wananasex but responsibly.. coz wanafundishwa elimu ya afya ya uzazi mapema.

Hapa kwetu binti akiwa na miaka 13 anaambiwa……, ‘Usicheze na wavulana ni mashetani wakubwa, na ole wako tukukute na wavulana, utahama hapa nyumbani’ Hapa binti anaanza kuwaona wavulana km viumbe hatari sn.!

Akiwa na miaka 20 wazazi wanamuambia ‘Kwa kweli Sisi wazazi wako hatumpendi yule mvulana unaefuatana nae’ binti anazidi kujiweka mbali na wanaume.. hapa ndo anaringa balaa.

Akiwa na miaka 25 wazazi wanaanza ‘Vipi mama? Kimya, hujatuletea mwenzio yoyote kututambulisha’ hapa ndo binti akifuatwa anadengua kidogo kumbe anataka.

Akiwa na miaka 28 wazazi wanakuja juu 'Wewe vipi wenzio wote wameolewa.. unasubiri nini’ hapa ndo kile kibinti kilichokua kinakuringia kinaanza kukutumia vitext vya kipuuzi.. mara mambo, mara nimekumiss.. umenimisd my foot??

Akiwa na miaka 30 wazazi wanasema 'Tumeshakuonya
acha kuchagua wanaume.. we vipi?’ binti anapanick.. anatamani kuolewa lakini alisharingaringa sana.

Akiwa na miaka 33 wazazi wanamuita kwa mazungumzo ‘Kuna mzee mmoja
kule Sumbawanga tumesikia anaweza kuondoa nuksi, twende tukupeleke’ binti anaanza kuwaza kuvuta mume kwa tunguri wakati aliringa mwenyewe.

Akiwa na miaka 38 wazazi wanamuita tena "Kuna Mchungaji Mabibo wanasema ukifunga wiki tu
unafunguliwa’ Binti anafunga na kuomba mara kubadilisha makanisa lakini hafanikiwi.

Akiwa na miaka 40 wazazi wanamuambia "kuna mzee mmoja kafiwa na mkewe anatafuta mke wa kumpunguzia mawazo.. unaonaje tukupe namba zake? Hata huyo ni sawa tu.. usichague sana.. tufariji wazee wako tuone japo kajukuu’

NB: GIRLS PLZ BE CARE.. KURINGA RINGA NI HATARI KWA MAISHA YAKO..

MISS TANZANIA 2014 NI SHEEDA


MISS TANZANIA 2014, BIBIE SITTI MTEMVU.

MSHINDI PAMOJA NA MSHINDI WA PILI BIBIE LILIAN NA WATATU JIHAN.

Mshindi wa Taji la Miss Tanzania 2014 azua maneno meengi katika mitandao ya kijamii, ikihusishwa uchakachuaji umechukua nafasi kubwa sana ktk jopo la majaji waliofanya maamuzi.
kwani baadhi ya watu wanadai kuwa hakustahili kulitwaa taji hilo kutokana na muonekano.
lakini mwisho wa siku majaji ndio waamuzi wa yote na hatimaye Bibie Sitti Mtemvu akalitwa taji hilo wakati nafasi ya pili ikishikiliwa na Bibie Lilian kamazima na nafasi ya tatu ilichukuliwa na Jihan Dimach..
hivyo tu yanii 

haya Bibie Siti Mtemvu ukatuwakilishe vyema Watanzania katika mashindano ya Dunia.

Saturday 11 October 2014

GADNER AFUTWA UMENEJA NA LADY JAYDEE


MTANGAZAJI maarufu wa redio, Gardner G. Habash kwa mara ya kwanza amefichua ukweli wa makubaliano waliyofikia na mwanamuziki maarufu nchini, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ ya kutozungumza na vyombo vya habari kuhusu taarifa zinazodai kuvunjika au kutengana kwao kindoa. Wakati Gardner akisita kueleza bayana kuhusu taarifa za kutengana kwake na Jide, taarifa ambazo gazeti hili limezithibitisha zinaeleza kwamba tayari mwanamuziki huyo ameshamuondoa ‘mumewe’ huyo katika nafasi ya umeneja ambayo amekuwa akiishikilia kwa miaka mingi sasa.

Meneja mpya wa Jaydee ambaye amerithi mikoba ya Gardner ni mwanamuziki wa miondoko ya ragga, Webiro Noel Wassira anayejulikana kisanii kwa jina la ‘Wakazi’. Wakazi ambaye alilithibitishia gazeti hili kwamba yeye ndiye meneja mpya wa Jide, anao uhusiano wa kindugu na mwanamuziki huyo ambaye nyota yake imekuwa iking’ara kwa miaka mingi sasa ndani na nje ya Tanzania.

Kwa upande wake, Gardner alipotakiwa kueleza kuhusu taarifa hizi, hakuwa tayari kuthibitisha zaidi ya kusema kwamba, Jide na yeye wote hawakuwa tayari kulizungumzia hili. “Ulitaka kujua kuhusiana na Jaydee au ulitaka kujua kuhusiana na mimi? Kama suala ni hilo, Lady Jaydee hayuko tayari kuzungumzia hilo kwa kuwa tumekubaliana kutolizungumzia hilo,” alieleza Gardner. Katika mahojiano hayo, Gardner ambaye ameishi na Jaydee katika ndoa waliyofunga kiserikali miaka tisa iliyopita, alishikilia msimamo wa kutotaka kueleza lolote kwa undani kuhusu undani wa mahusiano yake na Jide.

Mazungumzo kati ya Mwandishi wetu na Gardner yalikuwa kama ifuatavyo;

MTANZANIA Jumamosi: Kaka salama?, hapa ni chumba cha habari cha Magazeti ya New Habari (2006) Ltd. Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi za wewe kuachana na mkeo Jaydee na sasa jambo hili limethibitishwa na mmoja wa wanafamilia yenu, pengine hili sasa unalizungumziaje vipi Jaydee uko naye karibu?.

Gardner: Kwa sasa sipo karibu na Jaydee, nipo mbali naye maana nipo kazini, pili Jaydee mwenyewe hataki jambo hili nilizungumzie kwenye vyombo vya hbari na wala hayuko tayari kulizungumza.

MTANZANIA Jumamosi: Lakini wewe si ndiye meneja wake?

GADNA: Ulitaka kujua kuhusiana na Jaydee au ulitaka kujua kuhusiana na mimi juu ya Jaydee, kama suala la Lady Jaydee hayuko tayari kuzungumzia hilo kwa kuwa tumekubaliana kutolizungumzia hilo mimi wala yeye na sasa nipo kazini, basi.

Wakati Gardner akitoa kauli hizo tata, taarifa kutoka kwa watu walio karibu na wanandoa hao zinaeleza kuwa, kutengana kwa wawili hao kunatokana na kutofautiana kwao katika matumizi ya fedha, ulevi, na mmoja wao kutokuwa muaminifu wakati wakiwa ndani ya ndoa.

Taarifa hizo zinaeleza kwamba, licha ya wawili hao kutengana, bado hawajapeana talaka kwa sababu suala hilo ni la kisheria na wao bado hawajaamua kufika kwenye vyombo vya kisheria. “Wametengana na Lady Jaydee anajiandaa kuhamia katika nyumba yake nyingine ambayo aliionyesha katika kipindi chake cha ‘Diary ya Lady Jaydee’ akiwa anaifanyia usafi wakati Gardner naye anadaiwa kupanga maeneo ya Mwananyamala baada ya kuishi kwa ndugu zake kwa muda,” kilisema chanzo hicho. Wakati Wakazi akikiri kwamba yeye ndiye meneja mpya wa Jaydee hakuwa tayari kueleza lolote kuhusu ndoa ya nduguye na Gardner kwa maelezo kwamba yeye si msemaji wao katika masuala ya mapenzi na ndoa yao.

“Mimi sijui chochote, maana nilipokwenda Marekani niliwaacha wakiwa wachumba, lakini nilipokuwa huko nikasikia wameoana, niliporudi nikawakuta tayari wapo katika ndoa na nimeanza kazi ya umeneja wa Jaydee si muda mrefu, hivyo sijui mahusiano yao ya ndani labda muwaulize wenyewe,’’ alijibu Wakazi, lakini alipoombwa namba ya simu ya Jaydee anayoitumia sasa baada ya zile tulizonazo kutopatikana aligoma kuitoa. Hata hivyo, chanzo kingine kilidai kuwa, yeye kama mwanafamilia ya Lady Jaydee na Gardner ameheshimu makubaliano ya kutengana kwao.

Chanzo hicho kilidai kuwa hatua ya Gardner kuonekana kupitia kipindi cha Mikasi kinachorushwa na Kituo cha Chanel 5, ilitokana na kitendo cha Jaydee kukataa kwenda kwenye kipindi hicho akihofia kuulizwa swali hilo kuhusu ndoa yao.

“Baada ya waandaji wa kipindi cha Mikasi kumkosa Jaydee wakaamua kumualika Gardner” kilisema chanzo chetu hicho. Katika kipindi hicho cha Mikasi, Gardner alionyesha wazi kuwa na mgogoro na mke wake huyo, kwani kila alipoulizwa na mtangazaji wa kipindi hicho Salama Jabir kuhusiana na jambo lolote linalomuhusu Jaydee alikataa kulizungumzia huku akitaa kumuita mkewe, akitaka aitwe Jaydee.

Taarifa zinadai kuwa kuwa baada ya Jaydee kumtosa Gardner ameamua kumuweka ndugu yake huyo kuwa Meneja wake kwa kuwa yupo vizuri katika kujieleza. “Lakini pia ni mtu anayemfahamu muziki kwa mapana yake na pia ni mtu wa tungi (pombe) kama alivyokuwa meneja wake aliyeachana naye,” kilieleza chanzo hicho.

Chanzo hicho kilidai kuwa zamani Jaydee akigombana na mumewe alikuwa akitumia muda mwingi kulia na kumtungia nyimbo lakini kwa sasa ameamua kusimama peke yake na kufanya shughuli zake bila kukubali maumivu.

“Kwa sasa Jaydee si yule wa zamani aliyekuwa akilialia kila alipoumizwa, siku hizi Jaydee anajua kuvumilia na kusahau maumivu, kisha anaachana nayo na kufanya mambo mengine, Jaydee ni mpya siku hizi haliilii hovyo,’’ kilieleza chanzo chetu hicho.


Chanzo: Mtanzania (11/10/2014

Friday 10 October 2014

TAHADHARI ! UGONJWA MPYA KAMA EBOLA WA IBUKA NCHINI UGANDA


Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa tahadhari ya kusafiri nchini Uganda baada ya kuthibitishwa kuwa daktari mmoja amefariki kutokana na ugonjwa hatari wa Marburg unaosambazwa na popo.Kwa sasa Shirika hilo kwa ushirikiano na mamlaka za afya za Uganda wamemzuilia ndugu mmoja wa marehemu kwa hofu kuwa huenda naye aliambukizwa. Watu wengine zaidi ya 80, wakiwemo matabibu 38 waliokutana na mwenzao huyo siku kumi kabla ya kifo chake nao pia wanachunguzwa.

Kwa mujibu wa WHO na mamlaka za afya za Uganda, matokeo ya uchunguzi katika maabara ya Taasisi ya Utafiti wa Virusi kufuatia kifo cha tabibu huyo tarehe 28 Septemba yanathibitisha kwamba alifariki kutokana na homa hiyo hatari ya Marburg. Waziri wa Afya wa Uganda, Erioda Tumwesigye, alisema kuwa wizara yake inathibitisha daktari huyo aliyekuwa mtaalamu wa vipimo vya mionzi, alikufa kwa Marburg.Marehemu alikuwa tabibu katika Hospitali Kuu ya Wilaya ya Mpigi na alianza kuugua tarehe 17 Septemba akihudumu katika hospitali ya Mengo jijini Kampala, ambako alikuwa ameajiriwa mwezi mmoja uliopita. Inahofiwa kwamba katika kipindi cha wiki mbili kabla ya kifo chake alikutana na watu wengi wakiwemo matabibu wenzake pamoja na kwamba ni jamaa zake waliomzika.Kutokana na hilo, mwakilishi wa WHO nchini Uganda, Dokta Wondimagegnehu Alemu, alitahadharisha watu watu wanaoingia nchini Uganda, hasa katika wilaya ya Mpigi iliyo jirani na jiji la Kampala na pia Kasese alikozikwa marehemu. "Tunatoa tahadhari ya usafiri nchini Uganda baada ya kutambua kwamba mtu mmoja amefariki kutokana Marburg," alisema mwakilishi huyo ya WHO. Watu 80 wawekwa kwenye karantini.

Wizara ya afya ya Uganda pamoja na mashirika na taasisi nyengine husika zimechukua hatua za dharura mkiwemo kuwabaini na kuwatenga zaidi ya watu wapatao 80 waliokutana na mtu huyo aliyefariki kutokana na ugonjwa huo hatari wa Marburg.

Kwa mujibu wa wizara hiyo, watu hao watachunguzwa katika kipindi cha siku 21, ambazo ndiyo muda wa ishara za ugonjwa huo kujitokeza na kubainika na "yule atakayeonesha dalili hizo atasafirishwa moja kwa moja hadi kituo cha kitaifa cha kushughulikia magonjwa hatari," alisema Daktari Jane Aceng, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Huduma za Afya nchini Uganda, akiongeza kwamba wanafanya kila jitihada kuona kwamba wanamfuatilia kila mtu na "kuudhibiti ugonjwa huo mara moja kabla haujasambaa".

Popo husababisha Marburg Ugonjwa wa Marburg ni homa hatari inayonasibishwa na ugonjwa wa Ebola kwani virusi vya magonjwa hayo ni ya jamii moja ijulikanayo kama filoviridae.

Mnyama aina ya popo, ambao ni jamii ya mamalia wanaoruka na wanaoishi kwa kula matunda, ndiyo wanaosemekana kusambaza kirusi cha Marburg na maambukizi baina ya binadamu hutokana na kugusana kwa vidonda au majimaji yoyote kutoka kwa mgonjwa kama vile damu, mate, matapishi, kinyesi au mkojo wa aliyeambukizwa.

Miongini mwa dalili za ugonjwa huo ni pamoja na mtu kuwa na homa ya ghafla ya kiwango cha juu cha joto, maumivu ya kichwa, kutapika damu, maumivu ya viungo na misuli pamoja na kuvuja damu kutoka sehemu kadhaa kama vile machoni, puani, meno, masikioni, njia ya haja kubwa na hata kwenye ngozi. Aidha mtu aliyekumbwa na ugonjwa huo huharisha sana.

Kwa bahati mbaya, kama ilivyo kwa Ebola, ugonjwa huo nao haujapatiwa dawa maalum ya kuutibu wala chanjo dhidi yake. Wagonjwa hupewa tu dawa za kutuliza ishara husika.

Wataalamu wanaelezea kuwa viwango vya uwezekano wa mtu kufariki kutokana na ugonjwa huo ni kati ya asilimia 24 hadi 88, huku wakisisitiza njia za kujilinda na mgonjwa aliyekwishaathirika kuepuka kukutana kwa majimaji ya miili, damu, kinyesi au mate.

CREDIT TO: tanzaniatoday.co.tz

NA TUCHEKE

Karibuni Techeke...
angalia usivunje mbavu lakini..







KUCHEKA PIA IMO JAMANI