Thursday 3 May 2012

TUMSAIDIENI SAJUKI WATANZANIA

kushoto ni hali ya sajuki kwa sasa na kulia ni hali aliokua nayo kabla ya ugonjwa

Juma Kilowoko (SAJUKI) alivyo sasa

Msanii maarufu wa bongo movie Juma Kalowoko jina la kisanii SAJUKI yuko ktk hali mbaya na sisi km watanzania tunahitaji kumsaidia kwa chochote ulichokua nacho kwani anahitaji msaada mkubwa sana ili kukamilisha matibabu yake ambayo anatakiwa kwenda india kufanyiwa operation ya uvimbe alokua nao tumboni ambapo zinatakiwa Milioni 25 kwa ajili ya matibabu hayo ili kunusuru maisha yake .
Sajuki ambaye ni mume halali wa Wastara Juma ambaye pia ni mwigizaji anasema, kama wangekuwa na kiasi hicho cha pesa sasa hivi wangekuwa India kwani ugonjwa unaendelea kumtafuna mumewe kila kukicha.

"Sajuki anaumwa ndio maana tunawaomba wapenzi wetu na Watanzania wote, chochote walichonacho watuchangie ili tuweze kufika India kwaajili ya matibabu," anasema Wastara.
Wastara anasema hii itakuwa ni mara ya pili kwa Sajuki kwenda India kwamatibau, mara ya kwanza walienda na kupewa dawa ambazo madaktari waliamini zingeweza kumaliza tatizo.
"Tulikwenda mara ya kwanza na kupatiwa dawa ambazo ziliaminika kuwa zingemaliza tatizo, lakini imeonekana dawa haziwezi mpaka afanyiwe upasuaji,
Kufanyiwa upasuaji gharama zake ni kama milioni 25 za Tanzania, hapo bado usafiri malazi na vitu vingine vidogo vidogo,
Lakini kwetu la muhimu sasa hivi ni hizi milioni 25 za matibabu, hayo mengine mungu atatusaidia kikubwa uzima kwanza," anasema Wastara.
Aidha amesema ugonjwa unaomsumbua Sajuki ni kuwa na vivimbe kama matezi katika mishipa ya damu ambayo imekuwa aikiongezeka kila kukicha.
watanzania tunaomba msaada wenu kumsaidia kijana mwenzetu mtanzania mwenzetu,,

kupitia  AKIBA BANK A/C NO :050000003047
na MPESA kupitia NO:0762189592 jina litokee wastara juma.

No comments:

Post a Comment